MAAJABU YA DUNIA;ANGALIA PICHA YA MZEE AMBAYE HAJAOGA WA KUNAWA KWA MDA WA MIAKA 37!

***************************************************************
Mtazamo wa Maaskofu,Wainjilisti na Wachungaji kuhusu hali ya kisiasa kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015.
Maaskofu,Wainjilisti na Wachungaji wa madhehebu ya kipentecoste na Sabato Tanzania July 13 walikutana kwa ajili ya kuelezea mtazamo wao kuhusu hali ya kisiasa ya nchi yetu kuelekea uchaguzi mkuu unaotegemewa kufanyika 2015.
Maaskofu hao wakiongozwa na Askofu Mkuu wa kanisa la Jesus Power Miracle Joachim Peter Kimanza wamesema kwa sababu yameshatolewa matamko kadhaa na viongozi kuelekea uchaguzi mkuu na kwa changamoto hizo wamemtolewa mfano Mheshimiwa January Makamba.
Mfano wa January Makamba ambaye ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia umekuja baada ya kufanya mahojiano na kituo cha BBC London na kutangaza nia ya kuliongoza taifa la Tanzania muda ukifika.
Mbali na kumtaja January Makamba pia wametoa wito kwa vijana wengine wenye sifa za kugombea uongozi huo kujitokeza ili nao wawapime,wawatathmini pamoja na kuwapa ushauri na kuwaombea.
MAONI
Maaskofu,Wainjilisti na Wachungaji wa madhehebu ya kipentecoste na Sabato Tanzania July 13 walikutana kwa ajili ya kuelezea mtazamo wao kuhusu hali ya kisiasa ya nchi yetu kuelekea uchaguzi mkuu unaotegemewa kufanyika 2015.Maneno ya Rais Kikwete kuhusu ‘Urais’ wa January Makamba @JMakamba
Ifuatayo ni kauli ya Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete aliyoitoa Bumbuli Tanga kuhusu Naibu waziri ambae pia ni mbunge wa Bumbuli January Makamba.
Amenukuliwa akisema
>>> ‘January anafanya kazi nzuri ya ubunge pia ananisaidia sana kwa kazi ya wizara niliyompa, unajua January alipogombea Ubunge alinificha nilikuwa nasikia kwa wenzake tu pale ofisini, baadae alivyoweka mambo yake sawa ndio akaja kuniambia kwamba Mzee na Mimi najitosa’
‘Nikamtakia heri… kwa kweli kwa jinsi anavyohangaika na Jimbo lake inaonyesha Ubunge aliutaka kwa dhati kabisa ya kusaidia watu wa Bumbuli, nimesikia anafikiria mambo makubwa… hajaniambia mi nimesikia tu, namtakia kila la heri…. haya mambo anaamua Mungu wala hayalazimishwi’


‘Mungu akitaka linakuwa hata kama watu wote hawataki, Mungu akiwa hataki hata kama mtu ukitaka jambo hilo vipi haliwezi kuwa, mimi nilishauriwa na Mzee mmoja kwamba jambo likifika wakati wake utalipata hata kama utapingwa kiasi gani, kama halijafika wakati wake haliwezi kutokea, mimi niligombea 1995 sikupata kwasababu haikuwa wakati wake…. 2005 ikawa wakati wake nikapata, na wewe usipopata sasa usiweke nongwa” – JK
Hapa chini kuna video ya dakika 3 ikionyesha sehemu ya kazi zake Naibu waziri huyu ambae pia ni Mbunge wa Bumbuli kupitia CCM.





