Tuesday, July 22, 2014

Kauli ya Jeshi la Polisi Tanzania juu ya viungo vya binadamu vilivyopatikana July 21

polisiKama mfuatiliaji wa mitandao ya kijamii kuanzia usiku wa July 21 kulisambaa taarifa na picha zinazoonyesha viungo mbalimbali vya binadamu ambavyo vilitupwa katika daraja la Mpiji.
Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni ameongea na Power Breakfast ya Clouds Fm na kusema>>’Kweli tumekwenda tumevikuta viungo mbalimbali vya binadamu kama mikono,miguu,vichwa na viungo vingine’
‘Lakini vipo ndani ya mifuko ya sulphet na iko mifuko kama 80 hivi lakini tumechukua viungo hivyo na kuvipeleka hospital ya Muhimbili kwanza kuhifadhi na kwa ajili ya uchunguzi Mpaka sasa hakuna mtu aliyekamatwa’

Endelea Kusoma...

Monday, July 21, 2014

Kuhusu mtoto aliyepotea kwenye mazingira ya kutatanisha Dar es salaam.

mttTaarifa ya mtoto Marry ambaye kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii zimetolewa picha zake na maandishi ya kuwa amepotea kwenye mazingira ya kutatanisha na baadhi ya watu walisema kuwa walimuona amechukuliwa na mtu akawa anaelekea maeneo ya kanisa la Assemblies, Changanyikeni akiwa amepakiwa kwenye boda boda mpaka sasa hivi mtoto hajaonekana.

Endelea Kusoma...

Uliipata hii ya waumini wa kanisa Dar kupigana kanisani?

churchWaumini wa kanisa moja hapa Dar es salaam wamemaua kusitisha ibada baada ya kutokea ugomvi ambao umesababishwa na kutokuwepo kwa maelewano ambapo  walijigawana kimatabaka ya kuamua kila upande kuwa na mchungaji wao.
Hali imekua tofauti baada ya kusali nje kwa muda wa zaidi ya miezi miwili na sasa wameamua kurudi kusali kanisani upande wa juu na ndipo ilipotokea vurugu,Idara ya Hekaheka iko na stori kamili.

Endelea Kusoma...

Thursday, July 17, 2014

Hizi ni stori ambazo ukizisikia unaweza kushtuka kuona mt


knyHizi ni stori ambazo ukizisikia unaweza kushtuka kuona mtu anawezaje,sasa Unaambiwa kutoka katika mahakama kuu jijini Eldoret Nchini Kenya kuna mwanamke aliamua kuvua nguo ili kupinga uamuzi wa jaji kwenye kesi yake.
Kesi iliyokuwa ikimkabili mwanamke huyo ilikua ikuhusu mzozo wa ardhi dhidi yake na mwanamke mwingine ambapo wawili hao waliripotiwa kuoana na kwa mujibu wa desturi na mila za jamii ya wa Nandi inamruhusu mke kumuoa mke mwingine.
Mila hiyo huwa inazingatiwa endapo mwanamke aliyeolewa ameshindwa kupata watoto au kubainika kuwa tasa na pengine anahitaji kuendeleza kizazi katika familia aliyoolewa,hivyo mwanamke anayeolewa na mke mwingine haruhusiwi kua na uhusiano na mke aliyemuoa bali atatafuta mume atakaye zaa naye watoto.
Kwenye kesi Hakimu  Silah Munyao alikubaliana na hoja ya mlalamishi kuwa hakukua na ndoa na akatoa ruhusa ya kutimuliwa kwa mshtakiwa Hellen Tum [mkewe Tapkili Metto]kutoka kwa shamba hilo na kufidhiwa.
Kwenye kesi iliyowasilishwa mahakamani mwaka wa 2005,Tum alikua amemshtaki mumewe Tapkili Metto kwa kumkana licha ya kuishi naye kama mume na mke tangu mwaka 1989.
Hata hivyo Tapkili alikataa kuoana na Tum, Akiongeza kwamba yeye alikua msaidizi wa nyumba tu yaani Housegirl,hakimu munyao amesema hajaridhika na mashtaka kwa upande wa mshtakiwa kwamba watoto ambao Tum alimzalia Tapkili kwa kua hakukua na yeyote alisema alishuhudia ndoa baina ya wake hao wawili.
Muda mfupi baada ya uamuzi wa mahakama Bii Tum alivua nguo nje ya mahakama huku akimtukana hakimu kwa sauti ya juu kabla ya wapita njia kumtaka atulie

Endelea Kusoma...

Thursday, December 5, 2013

ABDU KIBA AKAMATWA AKIWA NA SIMU YA WIZI

KIJANA aliyefahamika kwa jina la Abdul Kiba amejikuta katika wakati mgumu baada ya kukamatwa akiwa na simu inayodaiwa kuwa ni ya wizi na ‘kuswekwa’ sero kufuatia jitihada za ndugu zake kumuwekea mdhamana kugonga mwamba, Ijumaa limetonywa.

Abdul Kiba.
Tukio hilo lilijiri Jumanne ya wiki hii katika viwanja vya Karume jijini Dar, wakati kijana huyo alipokuwa akicheza mpira.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini kilichokuwa uwanjani hapo, muda mfupi baada ya mchezo huo kumalizika, ndipo Abdu akawekwa chini ya ulinzi wa polisi wa kituo cha Msimbazi,  kwa tuhuma ya kuwa na simu ya wizi aina ya Samsung Galaxy yenye thamani ya  shilingi laki nane,  ambayo inadaiwa kuwa mali ya mfanyabiashara aliyetajwa kwa jina la Abdallah Muhidini.

Katika mahojiano yake na Polisi, Abdul alijitetea kuwa simu hiyo aliuziwa na vijana wawili siku za hivi karibuni aliowataja kwa majina ya Shaaban Rajab au Kibabu kama anavyojulikana kwa wengi (anayeshikiliwa na polisi).
Hata hivyo licha ya utetezi huo, Abdul alifunguliwa kesi jalada Na. MS/RB/12267/2013 WIZI KUTOKA MAUNGONI.
Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, ACP Juma Bwire alithibitisha kukamatwa Abdul Kiba na kwamba upelelezi bado unaendelea.

Endelea Kusoma...