Thursday, August 7, 2014

Hivi Unamchukuliaje Mpenzi Wako Mwenye Majibu Kama Haya Ukichat Nae

Eti ukiwa unachat mpenzi wako anakupa majibu kama haya unamchukuliajeee 
mfano 

1.ukimwambia kila ukimwambia bby i love you much au nakupenda sana mpenzi wangu 
yeye hujibu asante au thanks badala ya kusema i love you too mpenzi wangu 

2.ukimtumia vocha hukaa kimya ukimpigia hujibu asante nimeipataa. 

3.ukimwambia nimekumic mpenzi wangu hujibu asante au thanks au k thanks 

4.ukimwambia kuhusu sex huandika k au sawa au bila kujibu

jee unamuongeleajee mpenzi kama huyu kwa wale wataalamu saikolojia

Endelea Kusoma...

Thursday, July 24, 2014

Uliiona hii ya Joti baada ya Mkwe kumkatalia kuoa binti yake?

comedyJina lake lenye herufi nne ni miongoni mwa majina makubwa kwenye uigizaji wa vichekesho nchini Tanzania akiwa anatoka kwenye kundi la Orijino Komedi.
Tazama alichofanya hapa chini baada ya kukataliwa kumuoa binti aliemzimia.

Unavyomfahamu Joti, hiki kichekesho unakipa namba ngapi kwako toka umeanza kutazama vichekesho vyake mtu wangu?

 https://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=WOGgng2ZDR0

Endelea Kusoma...

Kuhusu Mjane aliyefukuzwa nyumbani baada ya mazishi ya mumewe

hkhhkKutoka kwenye Idara ya Hekaheka ina taarifa ya mjane aliyefukuzwa nyumbani kwa mumewe na ndugu wa marehemu zikiwa siku tatu baada ya mazishi ya mume wake,kanyang’anywa vitu kadhaa ikiwemo hati za nyumba na baadhi ya mali alizokuwa akimiliki na mumewe.

Endelea Kusoma...

Madaktari nchini India wametumia saa 7 kufanikisha upasuaji wa kinywa cha kijana Ashik Gavai mwenye umri wa miaka 17 aliyekuwa akipata maumivu ndani ya kinywani

Dr Sunanda Dhiware, mkuu wa Kitengo cha tiba ya meno katika hospitali ya JJ mjini Mumbai ameiambia BBC kuwa wamefanikiwa kuyang’oa meno 232 kinywani mwa Ashik aliyeletwa hospitalini hapo akiwa amevimba taya huku akilalamika kwa maumivu makali.
Madaktari wamesema wamelazimika kutumia nyundo na tindo kuyatoa meno hayo na wakadai kwamba hilo ni tukio la ajabu na linaingia katika rekodi ya dunia.Hata hivyo Upasuaji huo umehusisha jopo la madaktari wanne.
Dr Dhiware anasema katika uzoefu wake wa miaka 30 ya udaktari wa kinywa na meno hajawahi kukutana na tukio la namna hiyo. Ameongeza pia kuwa kulingana na vitabu vilivyopo vinasema hali kama hiyo inaweza kujitokeza katika taya la juu na meno yaliyowahi kung'olewa katika hali hiyo yalikuwa 37 lakini cha kushangaza ni kuwa tukio la Ashik Gavai limetokea katika taya ya chini na ameng'olewa meno 232 idadi ambayo ni kubwa huku akisalia na 28 kwa matumizi yake ya kawaida wakati kitaalamu mtu mzima anapaswa kuwa na meno 32.
Baba mzazi wa kijana Ashik ,Suresh Gavai amenukuliwa akisema mtoto wake alikuwa akilalamika kwa miezi kadhaa juu ya maumivu na kwamba walidhani inaweza kuwa ni matatizo ya saratani na ndipo wakamleta Mumbai.

Endelea Kusoma...

Wednesday, July 23, 2014

VIUNGO VYA BINADAMU VYAKAMATWA DAR ES SALAAM

 Fuvu
 Sehemu ya mguu
Vifurushi vya viungo vikiwa kwenye gari

Viungo mbali mbali vya binadamu vimekutwa katika eneo la kutupa taka la Bunju mjini Dar es Salaam katika mazingira ambayo haijafahamika mara moja kuwa viungo hivyo vimetoka wapi.
Kwa mjibu wa Afisa mmoja wa polisi ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema viungo hivyo vya binadamu vilivyokutwa ni miguu,vidole ambavyo vilikutwa vikiwa vimefungwa ndani ya mifuko.
Hata pamoja na viungo hivyo pia vifaa vya upasuaji vimekutwa zikiwemo glovuzi.
Mtu mmoja anashikiliwa kuhusishwa na tukio hilo ambaye ni dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo lililobeba viungo hivyo vya binadamu.
Haijafahamika mara moja miili hiyo ya binadamu imetolewa wapi na ilipelekwa eneo hilo kwa lengo gani.
Katika miaka ya hivi karibuni Tanzania imekuwa ikikabiliwa na tatizo la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi albino ambapo viungo vyao huchukuliwa,japo kuwa viungo hivi vilivyokutwa kwa sasa bado havihusishwi moja kwa moja na matukio ya mashambulizi na mauaji ya walemavu hao.

Endelea Kusoma...