MSANII filamu na muziki wa kizazi kipya wa Tanzania Baby
Joseph Madaha maarufu kwa jina la (Baby Madaha) amesema kwamba msanii mwenzake
wa muziki nchini,Naseeb Abdul maarufu kwa jina la Diamond Platinumz si msanii bali
ni mfanyabiashara.
Madaha amesema kwamba Diamond si mwanamuziki na kwamwe
huwezi kumlinganisha na msanii kama Barnaba Boy, anayefanya muziki kama sanaa
na kazi kulingana na kipaji chake na
kwamba Diamond si msanii wa muziki bali ni
msanii ngono anayefanya biashara ya muziki kupitia mapenzi.
Baby madaha ambaye hivi sasa yuko nchini Kenya kwa shuguli
za muziki amesema kwamba, Diamond hajui kuimba na ndiyo maana amekuwa msanii wa
matukio huku nyota yake ikiegemea kwenye mapenzi na wasichana wenye majina
makubwa hususn wasanii.
Akizungumza na kandili
yetu katika mahojiano maalum leo baby Madaha alisema kwamba,
"Binafsi niliposikia kwamba Diamond anaumiza kichwa kunasa penzi la msanii
Elizabeth Michael maarufu kwa jina la (Lulu) sikushangaa hata kidogo. kwa
sababu nilitambua kwamba soko lake la muziki limeanza kushuka hivyo lazima
atafute eneo lingine la kujiimarisha kibiashara, ili jina lake liendelee kuwika".
"Siku wanawake maarufu nchini Tanzania watakapo
jitambua na kuacha kulewa penzi la Diamond ndiyo itakayokuwa mwisho wa maisha
yake kimuziki,kwa sababu hatakuwa na jipya na hivyo soko lake litaanza
kuporomoka"alifafanua Baby Madaha
