Thursday, August 7, 2014

Hivi Unamchukuliaje Mpenzi Wako Mwenye Majibu Kama Haya Ukichat Nae

Eti ukiwa unachat mpenzi wako anakupa majibu kama haya unamchukuliajeee 
mfano 

1.ukimwambia kila ukimwambia bby i love you much au nakupenda sana mpenzi wangu 
yeye hujibu asante au thanks badala ya kusema i love you too mpenzi wangu 

2.ukimtumia vocha hukaa kimya ukimpigia hujibu asante nimeipataa. 

3.ukimwambia nimekumic mpenzi wangu hujibu asante au thanks au k thanks 

4.ukimwambia kuhusu sex huandika k au sawa au bila kujibu

jee unamuongeleajee mpenzi kama huyu kwa wale wataalamu saikolojia

Endelea Kusoma...

Thursday, July 24, 2014

Uliiona hii ya Joti baada ya Mkwe kumkatalia kuoa binti yake?

comedyJina lake lenye herufi nne ni miongoni mwa majina makubwa kwenye uigizaji wa vichekesho nchini Tanzania akiwa anatoka kwenye kundi la Orijino Komedi.
Tazama alichofanya hapa chini baada ya kukataliwa kumuoa binti aliemzimia.

Unavyomfahamu Joti, hiki kichekesho unakipa namba ngapi kwako toka umeanza kutazama vichekesho vyake mtu wangu?

 https://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=WOGgng2ZDR0

Endelea Kusoma...

Kuhusu Mjane aliyefukuzwa nyumbani baada ya mazishi ya mumewe

hkhhkKutoka kwenye Idara ya Hekaheka ina taarifa ya mjane aliyefukuzwa nyumbani kwa mumewe na ndugu wa marehemu zikiwa siku tatu baada ya mazishi ya mume wake,kanyang’anywa vitu kadhaa ikiwemo hati za nyumba na baadhi ya mali alizokuwa akimiliki na mumewe.

Endelea Kusoma...

Madaktari nchini India wametumia saa 7 kufanikisha upasuaji wa kinywa cha kijana Ashik Gavai mwenye umri wa miaka 17 aliyekuwa akipata maumivu ndani ya kinywani

Dr Sunanda Dhiware, mkuu wa Kitengo cha tiba ya meno katika hospitali ya JJ mjini Mumbai ameiambia BBC kuwa wamefanikiwa kuyang’oa meno 232 kinywani mwa Ashik aliyeletwa hospitalini hapo akiwa amevimba taya huku akilalamika kwa maumivu makali.
Madaktari wamesema wamelazimika kutumia nyundo na tindo kuyatoa meno hayo na wakadai kwamba hilo ni tukio la ajabu na linaingia katika rekodi ya dunia.Hata hivyo Upasuaji huo umehusisha jopo la madaktari wanne.
Dr Dhiware anasema katika uzoefu wake wa miaka 30 ya udaktari wa kinywa na meno hajawahi kukutana na tukio la namna hiyo. Ameongeza pia kuwa kulingana na vitabu vilivyopo vinasema hali kama hiyo inaweza kujitokeza katika taya la juu na meno yaliyowahi kung'olewa katika hali hiyo yalikuwa 37 lakini cha kushangaza ni kuwa tukio la Ashik Gavai limetokea katika taya ya chini na ameng'olewa meno 232 idadi ambayo ni kubwa huku akisalia na 28 kwa matumizi yake ya kawaida wakati kitaalamu mtu mzima anapaswa kuwa na meno 32.
Baba mzazi wa kijana Ashik ,Suresh Gavai amenukuliwa akisema mtoto wake alikuwa akilalamika kwa miezi kadhaa juu ya maumivu na kwamba walidhani inaweza kuwa ni matatizo ya saratani na ndipo wakamleta Mumbai.

Endelea Kusoma...

Wednesday, July 23, 2014

VIUNGO VYA BINADAMU VYAKAMATWA DAR ES SALAAM

 Fuvu
 Sehemu ya mguu
Vifurushi vya viungo vikiwa kwenye gari

Viungo mbali mbali vya binadamu vimekutwa katika eneo la kutupa taka la Bunju mjini Dar es Salaam katika mazingira ambayo haijafahamika mara moja kuwa viungo hivyo vimetoka wapi.
Kwa mjibu wa Afisa mmoja wa polisi ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema viungo hivyo vya binadamu vilivyokutwa ni miguu,vidole ambavyo vilikutwa vikiwa vimefungwa ndani ya mifuko.
Hata pamoja na viungo hivyo pia vifaa vya upasuaji vimekutwa zikiwemo glovuzi.
Mtu mmoja anashikiliwa kuhusishwa na tukio hilo ambaye ni dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo lililobeba viungo hivyo vya binadamu.
Haijafahamika mara moja miili hiyo ya binadamu imetolewa wapi na ilipelekwa eneo hilo kwa lengo gani.
Katika miaka ya hivi karibuni Tanzania imekuwa ikikabiliwa na tatizo la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi albino ambapo viungo vyao huchukuliwa,japo kuwa viungo hivi vilivyokutwa kwa sasa bado havihusishwi moja kwa moja na matukio ya mashambulizi na mauaji ya walemavu hao.

Endelea Kusoma...

Tuesday, July 22, 2014

Kauli ya Jeshi la Polisi Tanzania juu ya viungo vya binadamu vilivyopatikana July 21

polisiKama mfuatiliaji wa mitandao ya kijamii kuanzia usiku wa July 21 kulisambaa taarifa na picha zinazoonyesha viungo mbalimbali vya binadamu ambavyo vilitupwa katika daraja la Mpiji.
Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni ameongea na Power Breakfast ya Clouds Fm na kusema>>’Kweli tumekwenda tumevikuta viungo mbalimbali vya binadamu kama mikono,miguu,vichwa na viungo vingine’
‘Lakini vipo ndani ya mifuko ya sulphet na iko mifuko kama 80 hivi lakini tumechukua viungo hivyo na kuvipeleka hospital ya Muhimbili kwanza kuhifadhi na kwa ajili ya uchunguzi Mpaka sasa hakuna mtu aliyekamatwa’

Endelea Kusoma...

Monday, July 21, 2014

Kuhusu mtoto aliyepotea kwenye mazingira ya kutatanisha Dar es salaam.

mttTaarifa ya mtoto Marry ambaye kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii zimetolewa picha zake na maandishi ya kuwa amepotea kwenye mazingira ya kutatanisha na baadhi ya watu walisema kuwa walimuona amechukuliwa na mtu akawa anaelekea maeneo ya kanisa la Assemblies, Changanyikeni akiwa amepakiwa kwenye boda boda mpaka sasa hivi mtoto hajaonekana.

Endelea Kusoma...

Uliipata hii ya waumini wa kanisa Dar kupigana kanisani?

churchWaumini wa kanisa moja hapa Dar es salaam wamemaua kusitisha ibada baada ya kutokea ugomvi ambao umesababishwa na kutokuwepo kwa maelewano ambapo  walijigawana kimatabaka ya kuamua kila upande kuwa na mchungaji wao.
Hali imekua tofauti baada ya kusali nje kwa muda wa zaidi ya miezi miwili na sasa wameamua kurudi kusali kanisani upande wa juu na ndipo ilipotokea vurugu,Idara ya Hekaheka iko na stori kamili.

Endelea Kusoma...

Thursday, July 17, 2014

Hizi ni stori ambazo ukizisikia unaweza kushtuka kuona mt


knyHizi ni stori ambazo ukizisikia unaweza kushtuka kuona mtu anawezaje,sasa Unaambiwa kutoka katika mahakama kuu jijini Eldoret Nchini Kenya kuna mwanamke aliamua kuvua nguo ili kupinga uamuzi wa jaji kwenye kesi yake.
Kesi iliyokuwa ikimkabili mwanamke huyo ilikua ikuhusu mzozo wa ardhi dhidi yake na mwanamke mwingine ambapo wawili hao waliripotiwa kuoana na kwa mujibu wa desturi na mila za jamii ya wa Nandi inamruhusu mke kumuoa mke mwingine.
Mila hiyo huwa inazingatiwa endapo mwanamke aliyeolewa ameshindwa kupata watoto au kubainika kuwa tasa na pengine anahitaji kuendeleza kizazi katika familia aliyoolewa,hivyo mwanamke anayeolewa na mke mwingine haruhusiwi kua na uhusiano na mke aliyemuoa bali atatafuta mume atakaye zaa naye watoto.
Kwenye kesi Hakimu  Silah Munyao alikubaliana na hoja ya mlalamishi kuwa hakukua na ndoa na akatoa ruhusa ya kutimuliwa kwa mshtakiwa Hellen Tum [mkewe Tapkili Metto]kutoka kwa shamba hilo na kufidhiwa.
Kwenye kesi iliyowasilishwa mahakamani mwaka wa 2005,Tum alikua amemshtaki mumewe Tapkili Metto kwa kumkana licha ya kuishi naye kama mume na mke tangu mwaka 1989.
Hata hivyo Tapkili alikataa kuoana na Tum, Akiongeza kwamba yeye alikua msaidizi wa nyumba tu yaani Housegirl,hakimu munyao amesema hajaridhika na mashtaka kwa upande wa mshtakiwa kwamba watoto ambao Tum alimzalia Tapkili kwa kua hakukua na yeyote alisema alishuhudia ndoa baina ya wake hao wawili.
Muda mfupi baada ya uamuzi wa mahakama Bii Tum alivua nguo nje ya mahakama huku akimtukana hakimu kwa sauti ya juu kabla ya wapita njia kumtaka atulie

Endelea Kusoma...

Thursday, December 5, 2013

ABDU KIBA AKAMATWA AKIWA NA SIMU YA WIZI

KIJANA aliyefahamika kwa jina la Abdul Kiba amejikuta katika wakati mgumu baada ya kukamatwa akiwa na simu inayodaiwa kuwa ni ya wizi na ‘kuswekwa’ sero kufuatia jitihada za ndugu zake kumuwekea mdhamana kugonga mwamba, Ijumaa limetonywa.

Abdul Kiba.
Tukio hilo lilijiri Jumanne ya wiki hii katika viwanja vya Karume jijini Dar, wakati kijana huyo alipokuwa akicheza mpira.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini kilichokuwa uwanjani hapo, muda mfupi baada ya mchezo huo kumalizika, ndipo Abdu akawekwa chini ya ulinzi wa polisi wa kituo cha Msimbazi,  kwa tuhuma ya kuwa na simu ya wizi aina ya Samsung Galaxy yenye thamani ya  shilingi laki nane,  ambayo inadaiwa kuwa mali ya mfanyabiashara aliyetajwa kwa jina la Abdallah Muhidini.

Katika mahojiano yake na Polisi, Abdul alijitetea kuwa simu hiyo aliuziwa na vijana wawili siku za hivi karibuni aliowataja kwa majina ya Shaaban Rajab au Kibabu kama anavyojulikana kwa wengi (anayeshikiliwa na polisi).
Hata hivyo licha ya utetezi huo, Abdul alifunguliwa kesi jalada Na. MS/RB/12267/2013 WIZI KUTOKA MAUNGONI.
Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, ACP Juma Bwire alithibitisha kukamatwa Abdul Kiba na kwamba upelelezi bado unaendelea.

Endelea Kusoma...

DOCTOR ANASWA AKILA URODA NA BINTI ALIYEKUWA AKIMTOA MIMBA..!! NO NO NOMA SANA..!!


theclicktz.com/
Inasemekana imekuwa ni tabia ya huyu jamaa kutimiza haja zake pindi anapopata kichwa cha kutoa mimba, pamoja na kuwa huwa analipwa kutokana na kazi hiyo ya kutoa mimba ila huwa anaomba uroda mara kabla hajaanza kazi hiyo.

Endelea Kusoma...

Dunia yaomboleza kifo cha Mandela

Tanzania imetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia tarehe 6 hadi 8 Desemba, 2013, kufuatia kifo cha rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.
Rais Jakaya Kikwete wa nchi hiyo pia ameagiza kuwa katika kipindi hicho cha siku tatu bendera zote zitapepea nusu mlingoti.
Kufuatia kifo hicho Rais Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini na kupitia kwake kwa mkewe Bi Graca Machel, wanafamilia wote na wananchi wote wa Afrika ya Kusini kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela kilichotokea tarehe 5 Desemba, 2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Rais ameuelezea msiba huu kuwa ni msiba mkubwa kwetu sote.
"Afrika ya Kusini, Afrika na dunia kwa ujumla imepoteza mtu mashuhuri na shujaa mkubwa wa Karne ya 20 na 21.Tunaelewa machungu waliyonayo wananchi wa Afrika ya Kusini kwa kupoteza kiongozi shupavu, jasiri, mwana mapinduzi , mvumilivu na mstahimilivu". Ameongeza Rais Kikwete.
Rais amemuelezea Mzee Mandela kuwa ni kielelezo cha aina yake kwa wanadamu kwa moyo wake wa kusamehe, huruma na upendo uliomwezesha kuwaunganisha wananchi wa Afrika ya Kusini kuwa taifa moja baada ya kipindi kirefu cha mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.
"Mandela ni mfano bora kwa wanadamu wa jinsi binadamu muungwana anavyopaswa kuwa . Ni wajibu wa wana Afrika Kusini, Afrika na dunia kuiga mfano wake hasa moyo wake wa uzalendo, kujitolea hata maisha yake kwa ajili yake na wananchi wenzake". Rais ameongeza kusema, "Tuzidi kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mzee Mandela mahali pema peponi".
Mandela amefariki huko Johannesburg akiwa na umri wa miaka 95 na yeye ndiye aliyeiongoza Afrika Kusini kutoka mikononi mwa watawala wa ubaguzi wa rangi baada ya kufungwa jela kwa miaka 27.
Mandela alikuwa anatibiwa homa ya mapafu nyumbani kwake baada ya kulazwa hospitalini kwa miezi mitatu.
Katika taarifa yake kwa watu wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, alisema kuwa Mandela amewaaga lakini yuko mahali salama.
Rais Zuma amesema kuwa taifa limepoteza mtu waliyemjua kama mtoto wa taifa hilo.
Mandela aliwahi kushinda tuzo ya amani ya Nobel, na kutambulika kama rais aliyeheshimika sana hasa kwa kupatanisha watu wa Afrika Kusini baada ya kutoka gerezani.



Endelea Kusoma...

BELLE 9 AFUMANIWA NA MKE WA MTU...!! SOMA STORI NZIMA HAPA...!!



Mkali wa bongo fleva Abelnego Damian 'Belle 9' Aliwahi kukumbwa na zahma mbaya ya kufumaniwa chumbani na mke wa mtu jambo ambalo lilimalizwa kwa kuminywa chini kwa chini lakini habari hiyo haikubumburuka wala kulipotiwa mahali popote. Kwa mujibu wa chanzo chetu makini ambacho pia ni msanii mkubwa katika game la muziki (jina lipo kwenye droo zetu) Bele alipata kashfa hiyo mwaka 2010 ambapo siku ya tukio alikuwa chumbani kwake na mwanamke huyo ambaye hakujua kama ni "mali ya mtu" Aidha "mtonyaji" wetu alizidi kuweka bayana kuwa, bahati nzuri Belle 9 alikuwa anafahamiana vyema na mfumaniaji huyo ambapo alikuwa muungwana kwa kuomba msamaha huku akiipoza ishu hiyo kwa  misimbazi kadhaa "ishu haikuwa ya kitoto . Waliyamaliza chumbani humo humo lakini Belle 9 alivunja kabisa uhusiano wa aina yeyote na mwanamke huyo. Mdakuzi wetu alipomtafuta Belle 9 kwa njia ya simu , alikiri kukumbwa na jambo hilo huku akisisitiza kulisahau. "Duh! hiyo ni kitambo sana ujue, ila anyway ni kweli lakini halikuwa fumanizi kama unavyosema, wala hakuwa mke wa mtu zaidi ya mapenzi ya kawaida" alisema Belle 9.

Endelea Kusoma...

BREAKING NEWS:MTAA WAFUNGWA, SOMA HAPA KUJUA SABABU NI NINI

Kundi la muziki kutoka nyanda za juu kusini linaloudwa na lucky junior ,samaiko ,leby cute,etco the best siku ya leo mda mfupi uliopita wameifunga mitaa  ya Mwanjelwa katika maeneo ya maduka makubwa ya nguo magari yameshindwa kupita wala pikipiki walipokuwa wakienda kununua viwalo kwa ajiri ya ngoma yao mpya iitwayo fine. Ikumbukwe kwamba Afro Magic ndo wale vijana waliofanya hit ya Mihogo tupogo rmx ilikuwa ni full patashika maana wananchi walijazana kuwa tazama na wengine walisikika wakisema tuimbie kidogo  kwa kweli vijana hawa n kiboko atakama wanasema nabii hakubariki kwao hii imekuwa tofauti maana wananchi walifwata vijana hawa kila sehemu ili wapate kusikia wakiimba

Endelea Kusoma...

Nchimbi abebeshwa zigo la Prof Kapuya

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi ameingia lawamani kwa kudaiwa kumlinda Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), anayedaiwa kumbaka na kumtishia kumuua binti wa miaka 16.
Akizungumza kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi wa simu (sms) na Tanzania Daima jana, binti anayelalamika kutishiwa maisha na Profesa Kapuya, amemtuhumu Waziri Nchimbi kushindwa kulishughulikia suala hilo mapema licha ya kuwa na taarifa za tukio hilo muda mrefu.
Binti huyo alisema kuwa Dk. Nchimbi ni miongoni mwa mawaziri na viongozi wa CCM waliokuwa wakifahamu kila kinachoendelea dhidi ya malalamiko husika.
Alibainisha kuwa makada hao wa CCM walikuwa wakifanya jitihada za kuhakikisha manyanyaso na vitisho kutoka kwa Profesa Kapuya haviwekwi hadharani.
Katika kile kinachoonekana ni kukata tamaa juu ya usalama wake pamoja na dada yake, binti huyo alisema amewasiliana na Waziri Nchimbi asubuhi ya jana na kwamba waziri huyo hakuonyesha dalili yoyote ya kujali madhila yao.
Alisema kutokana na Waziri Nchimbi kutokutilia uzito malalamiko yao, waliamua kumuandikia ujumbe mfupi wa maandishi wakimshutumu kuendelea kumlinda Profesa Kapuya.
“Nimemwambia katika ujumbe mfupi wa maneno (sms) kuwa jukumu la polisi iliyo chini ya wizara yake ni kuhakikisha wananchi wanalindwa dhidi ya manyanyaso na vitisho vya aina yoyote, na kwamba katika kadhia hii ya Kapuya Jeshi la Polisi limekuwa kimya.
“Matukio mbalimbali ya kihalifu yenye kutatanisha yametokea nchini, lakini serikali inasema haiwajui wahusika na kwamba hata hili la kutishiwa maisha pia serikali inasubiri nife,” alisema binti huyo.
Binti huyo alisema katika ujumbe huo aliomtumia Waziri Nchimbi, pia amemdokezea kuwa haogopi kitakachompata ilimradi yupo katika msitari wa kutafuta haki yake.
Amedai kuwa hivi sasa bado kuna jitihada kubwa za watu walio karibu na Kapuya kuwataka waachane na suala hilo.
“Juzi mtu aliye karibu na Kapuya ametuhoji tunataka nini ili tuachane na jambo hili… sisi tumemjibu tunataka haki si kingine chochote,” alisema.
Jitihada za Tanzania Daima kumpata Waziri Nchimbi ziligonga mwamba baada ya simu yake ya mkononi kuita bila majibu na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno (sms) haukujibiwa.
Wanaharakati walia na polisi
Wakati sakata hilo la Kapuya likiwa kwenye hali ya kutoeleweka, baadhi ya wanaharakati na watetezi wa masuala ya jinsia wamelitaja Jeshi la Polisi kwa kuchangia vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya Siku ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia kwenye viwanja vya Mtandao wa Jinsia (TGNP).
Joseph Mathias, alisema vitendo hivyo vya ukatili vinaongezeka kutokana na polisi kuwalea na kuwalinda baadhi ya vigogo wanaovitenda.
Bila kumtaja jina, Mathias alisema hivi karibuni kiongozi mmoja anahusishwa na ubakaji na kutishia kuua, lakini hadi sasa hajafikishwa mahakamani.
Mathias, alisema pamoja na dawati la kupinga ukatili wa kijinsia kupata taarifa hiyo, lakini hadi leo halijamchukulia hatua yoyote ile kama inavyofanya kwa watu wengine waliofanya makosa kama hayo.
Aliongeza kuwa polisi bado ni tatizo katika mapambano hayo, na kama hawatabadilika kiutendaji kuna uwezekano tatizo hilo likazidi kushamiri.
“Kushindwa kuwachukulia hatua za kisheria watu kama hawa, kumekuwa chanzo cha baadhi ya watu kuyachukulia matendo haya ya ukatili wa kijinsia kuwa ni haki yao,” alisema Mathias.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa TGNP, Anna Sangai, alisema changamoto kubwa inayochangia vitendo hivyo katika jamii ni mila potofu.
“Sisi TGNP tunalichukulia kuwa ni la kirasilimali, hivyo tunaishauri serikali ijaribu kutenga fedha za kutosha na kuzielekeza kwenye Wizara za Mambo ya Ndani ya Nchi na Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto ili zifikishe elimu bila vikwazo kwa jamii,” alisema.
Anna alisema endapo jamii itapatiwa elimu kuhusu ukatili huo, anaamini kuwa vitendo hivyo kwa kiasi kikubwa vitapungua.
Aidha, jamii nayo imetakiwa kuondokana na mila potofu kwa kuwaona wanawake si lolote katika kuchangia masuala mbalimbali ya kimaendeleo.
Mwakilishi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Judith Kizenga, alisema serikali imejipanga kukamilisha sheria zote ambazo zitaweza kupambana na kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii.
Kuruthumu Mikidadi, ambaye ni mwakilishi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, alikiri kuwa dawati la jinsia linakabiliwa na changamoto mbalimbali, lakini hali hiyo inatokana na uchanga wake.
Awali kwa nyakati tofauti, washiriki zaidi ya wanne kutoka mikoa ya Mbeya, Morogoro na Dar es Salaam, walilishambulia dawati hilo kuwa watendaji wake wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya rushwa na kushindwa kutoa haki.
Walisema wakati mwingine mhalifu anamfikishwa kwenye dawati hilo, lakini cha kushangaza kesho unamkuta ameachiwa katika mazingira tata.

Endelea Kusoma...

Slaa: CHADEMA si legelege

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa,


amesema kamwe chama hicho hakitakubali kuwa legelege katika kusimamia misingi yake, ikiwemo katiba inayowaunganisha wanachama wote. Alisema kuwa licha ya kuzushiwa propaganda nyingi ikiwemo udini na ukabila, lakini chama hicho kimefanikiwa kuzishinda hali aliyoelezea imewakomaza katika safari yao ya kuchukua madaraka.
Kauli hizo alizitoa jana mjini Kahama mkoani Shinyanga alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya CDT, ikiwa mwanzo wa ziara yake ya kukiimarisha chama.
Dk. Slaa alisema wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2010, chama hicho kiliwaahidi Watanzania kuwa kama kingeshika dola, kingekuwa imara kusimamia serikali itakayowatumikia wananchi.
Alibainisha kuwa ili kuitimiza ahadi hiyo, chama hicho kamwe hakiwezi kuwa legelege kwa wanachama na viongozi wasiotaka kufuata katiba na taratibu za chama.
“Watanzania tulieni, tulieni, tulieni. Chama hiki kipo kwa ajili ya kuwatumikia ninyi na kusimamia maslahi yenu. Acheni ushabiki kwenye masuala mazito,” alisema.
Dk. Slaa alisema amekuwa akipigiwa simu na watu wengi wakimuulizia hali ya mambo inavyokwenda ndani ya chama hicho, hasa baada ya uamuzi wa Kamati Kuu kuwavua uongozi baadhi ya makada wake akiwemo mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.
“Mimi nawaambia watulie tu… Nawaambia waviamini vikao vya chama chao, ndani ya CHADEMA hakuna mtu mkubwa kuliko katiba. Wote hapa tunaunganishwa na katiba.
“Chama hiki kimepita kila aina ya propaganda ikiwemo hii ya juzi ya ugaidi, zote tumezishinda na tutaendelea kuzishinda. Hata hii ya sasa inayosukumwa na mipango ya hujuma inayopangwa na CCM, wakishirikiana na vyombo vya dola na watendaji wa serikali, tunazidi kuimarika na kutukomaza kwenda kushika dola.
“Wakati wa kampeni mwaka 2010 tuliwaambia Watanzania kuwa tunakwenda kusimamia maslahi ya Watanzania. Tulisema elimu bure, mwaka jana wameamua kutuiga, tulisema vifaa vya ujenzi vishuke, pia wameamua kutuiga, lakini wameshindwa kutekeleza,” alisema.
Dk. Slaa alisema kuwa CCM wameshindwa kutekeleza kile kilichokuwa kikisemwa na CHADEMA, ambayo sasa inaamini ikiingia madarakani itatimiza mambo iliyowaahidi wananchi.
Safari yapata matatizo
Ziara ya Dk. Slaa jana iliingia dosari baada ya magari aliyokuwa akiyatumia kupata hitilafu za kiufundi zilizosababishwa na kile kinachodaiwa ni mafuta machafu waliyoyaweka katika kituo kimoja cha mafuta kilichopo wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Mafuta hayo yaliyafanya magari yaliyokuwa kwenye msafara huo kushindwa kwenda mwendo uliotarajiwa, na hivyo kusababisha Dk. Slaa na timu yake kufika katika viwanja vya mkutano saa 12 jioni.
Dk. Slaa leo anatarajia kwenda mkoani Kigoma ambako atahutubia

Endelea Kusoma...

DIAMOND AHOJIWA KINGEREZA NCHIN KENYA, SOMA HAPA UONE KINGEREZA CHA DIAMOND

Tanzanian ‘My Number One’ hitmaker Diamond Platinumz made an appearance on Coke Studio Africa this past weekend. We had the chance to catch up with him and talk to him about his music and his style.
Here’s what he had to share:
What inspired the name Diamond?

The name Diamond really started as a joke while I was singing in Wasafi before I became famous. In the beginning, I didn’t like the name and I would get annoyed every time I was referred to as Diamond. As a musician it can be a bit difficult to change your name last minute. Getting people used to your new name is an uphill task that I wasn’t ready to undertake. Since the name had stuck and I already had a large fan base that knew me as Diamond, I decided to maintain it.
How would you describe your music?
I describe my music as Bongo Flava. It’s a mixture of Afro Pop, R&B, hip hop and Arabic flavor.
What inspires your music?
I get my inspiration from the society and through my own life experiences.
Which musician inspires you and why?
I am inspired by Usher Raymond because of his undeniable vocal prowess and his breathtaking performances. Usher started singing at a tender age and despite the changing times, he has managed to retain his place as one of the greatest R&B musicians of all time. Usher is one guy I would like to collaborate with in the near future.
You are an award winning musician, how does that feel?
It feels great! I mean it shows that my fans appreciate what I am doing. I spend a lot of time in the studio with the hope of producing hit songs. The more I get awarded, the more pressure I get to remain relevant in the ever changing music industry. You know music is very dynamic, what was cool or hot last year is obviously not this year. I always ensure I stay abreast with the new music trends. Perhaps that is the reason I always scoop various awards.
What’s your biggest achievement?
I have achieved a lot! I thank God for my success so far, it wasn’t easy. Despite the fact that my mother can take care of herself, just being able to cater for her expenses on her behalf brings me great joy. I consider that as my biggest achievement. A lot of people make it and forget where they came from but not me, the place my mother holds can never be taken over by fame, money or my music career in general.
Tell me a bit more about your mother
Singing is one of the most fulfilling ways I express myself, and my mother had the necessary starting tools to help me. I started singing at tender age like Usher (laughs), and if my memory serves me right I remember I was in class five and by then. I couldn’t write my own lyrics therefore I would do an impression of some songs and practice repeatedly until I got the lyrics right. However my mother saw the talent in me and eventually she started writing lyrics for me. She always encouraged me to open my mouth in front of others and sing. It seems obvious but it takes a lot of courage, enormous desire and passion to sing in public. My mother instilled all the necessary requirements I needed to succeed in the music industry in Tanzania. She has played a very huge role in my life; she was and still is my mentor to date. Once I got to high school, my mother asked me to focus more on my studies and to put music aside. Nonetheless I continued writing and singing secretly because I felt as though music was my destiny.  As soon as I was done with secondary school, I remember I had to sell a ring my mother had given me to enable me to get a recording deal. Making it wasn’t as easy as it seems now. Then I had to lie to her that the ring had dropped into the pit hoping and praying that the songs I had recorded hit. Unfortunately selling the ring bore no fruits because those songs didn’t make it to the corridors of any radio station. Luckily, I met Papa Misifa who had heard my songs and from there, my music took a turn for the better. We released my first hit Nenda Kamwambie in 2009 and the rest is history.
What are your future plans?
Music is my main source of income currently but you never know what tomorrow holds for you. I have ventured into various businesses on the side to ensure I remain financially stable just in case I am unable to sing or dance in future (God forbid). I own a recording label called WCB where I manage and mentor a couple of upcoming artists. My main aim is to take the Tanzanian music industry into further heights.
How is the Tanzanian music industry?
The Tanzanian music industry is just like any other industry. There’s cut-throat competition among artists, a lot of imitation also, so you really have to strive to excel. However I think the competition is healthy as it keeps us (musicians) on our toes and also enables us to produce enjoyable and entertaining music.
What does music mean to you?
Music means a lot to me! Apart from earning me a living, music also gives me some sort of fulfillment. Money is secondary to me and has never been my main motivation to sing. Though nowadays the pursuit of money is almost directly linked to the pursuit of happiness. Many people argue that money is equal to happiness. However this mindset has led many people down a path that doesn’t suit them leaving them frustrated at their work places. The secret is to follow your dream, or pursue something you are good at and you will definitely succeed.

Endelea Kusoma...

MAAJABU: MAPACHA WAKIUME NA WAKIKE WAFUNGA NDOA SIKU MOJA NA KUINGIA KWENYE GUINNESS BOOK OF WORLD RECORDS

Couple mbili za mapacha wanne wanofanana (identical twins) wa Nigeria, wamefanya kile kinachoaminika kuwa ni cha kipekee na cha kwanza kuwahi kufanyika nchini humo, baada ya kufunga ndoa zao siku moja na kufanya sherehe moja.
twin wed-1
Mapacha hao wa kiume (Febisola Kehinde Okunniyi na Chibuzor Adelakin Okueze) walifunga ndoa na wapenzi wao mapacha wa kike (Folawemi Taiwo Okunniyi na Chinonso Akinade Okueze) Jumamosi iliyopita (Nov 30) huko Lagos, Nigeria.
twin wed-2
twin wed-3
Mtandao wa Daily Star wa Nigeria umedai kuwa ndoa za mapacha hao wanne kwa pamoja huenda zikawa za kwanza kwa Afrika, na kwa mujibu wa maafisa wa kitabu cha rekodi za dunia ‘Guinness Book of World Records’, ni ya 251 duniani.

Endelea Kusoma...

Wednesday, December 4, 2013

MASIKINI MWANAFUNZI AULIWA NA MPENZI WAKE, SOMA KUJUA SABABU


Na Waandishi Wetu
KIFO cha kikatili cha mwanafunzi aliyeuawa siku chache baada ya kuhitimu kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Luguruni na mkazi wa Kimara Golani, Dar, Sharifa Rajab (18) bado ni simanzi nzito katika familia yake.

Sharifa aliuawa kikatili Novemba 22, mwaka huu, Kimara Golani jijini Dar na mtu anayedaiwa ni mpenzi wake ajulikanaye kwa jina la Abdul (22) ambaye ni dereva wa bodaboda.
SIMULIZI YENYE MAJONZI
Akizungumza kwa masikitiko makubwa, baba wa marehemu, Rajab Abdallah alisema siku ya tukio asubuhi, yeye na mke wake wakiwa kazini, Sharifa aliondoka nyumbani hapo  bila taarifa na kuwaacha wadogo zake tu.
“Tuliporudi jioni, mimi na mama yake tulianza kuhangaika kumtafuta bila mafanikio. Mwisho tuliamua kurudi kulala japokuwa usingizi ulikataa. Unajua tena mtoto ni mtoto. Huwezi kupata usingizi wakati mwanao hujui aliko.

“Tulipanga siku iliyofuata kwenda kutoa taarifa polisi, lakini ilipofika saa kumi na moja alfajiri, tuliletewa ujumbe kwamba kuna mwili wa mwanamke umekutwa kwenye chumba cha jirani.
“Ilikuwa vigumu kusema kwamba mwili huo ni wa mtoto wetu Sharifa, tuliamini kifo kipo, lakini watakufa wengine si mtoto wetu Sharifa.

“Hata hivyo, tulifunga safari kwenda kuuangalia mwili huo. Sikuamini hata kidogo nilipogundua kwamba ni mwanangu ndiye alilala kitandani, amekufa kwa kuchomwa kisu kooni na kwenye mbavu zote, kitanda chote kilijaa damu. Sharifa alikuwa si Sharifa tena bali marehemu Sharifa,” machozi yanamlengalenga.
Anaendelea: “Inaniuma sana! Mbaya zaidi nilijua  chumba hicho ni cha  kijana ambaye ni dereva wa bodaboda, anaitwa Abdul. Nikajiuliza ina maana alikuwa ni mpenzi wake? Sikupata jibu.”
TABIA YA MAREHEMU
Baba wa marehemu aliongeza kuwa, kwa kipindi chote cha uhai, Sharifa  hakuwahi kuonesha dalili kwamba alikuwa katika uhusiano wa kimapenzi, alikuwa ni msiri sana.

MTUHUMIWA WA MAUAJI AACHA UJUMBE
Habari zaidi zilidai kuwa, baada ya mtuhumiwa huyo kutekeleza mauaji ya binti huyo aliacha ujumbe wa maandishi akisema kuwa watu wasihangaike kumtafuta kwani na yeye anakwenda kujiua.
Hata hivyo, mtuhumiwa hakwenda kujiua, badala yake alifika Kituo Kikuu cha Mabasi ya Mikoani (UBT) kutafuta usafiri wa kurudi kwao Tanga lakini alipokosa aliamua kujisalimisha katika Kituo cha Polisi Ubungo na kukiri kuua.

Mmoja wa viongozi wa serikali ya mtaa (hakutaka kutaja jina lake) alisema mtuhumiwa huyo alipohojiwa polisi alisema hajui kilichotokea, akaomba apewe nafasi akamzike mpenzi wake huyo.
KAMANDA WA POLISI
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni,  ACP Camilius Wambura alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo ambapo alisema kwa mujibu wa mtuhumiwa alifanya kitendo hicho kutokana na wazazi wa msichana huyo kukataa yeye asimuoe na tayari alikuwa na mchumba mwingine.

Marehemu Sharifa alizikwa Novemba 24, mwaka huu katika Makaburi ya Golani Nzasa, Dar. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina.

Endelea Kusoma...

HATARIII...Tajiri agonganisha wanawake uwanja wa ndege WA JULIUS NYERERE

Na Richard Bukos
MWANAUME mmoja aliyeelezwa kuwa ni tajiri mwenye nazo mjini, amezua tafrani na kusababisha timbwili la nguvu kwa dakika kadhaa baada ya kugonganisha wanawake wawili waliodaiwa kuwa chini ya miliki yake kwa wakati mmoja, subiri hapohapo tukujuze!
Mtiti huo uliovuta hisia za wengi ulichukua nafasi Ijumaa iliyopita, mishale ya saa sita na dakika zake usiku, pande za Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ‘JNIA’ ambapo
mwanaume huyo ambaye jina lake halikupatikana mara moja alitua na Ndege ya Shirika la Kenya.
ANGALIA SINEMA
Hali ya hewa ilikuwa ya kuridhisha kabisa katika eneo la uwanja wa ndege wakati paparazi wetu akiwa kwenye sehemu maalum ya kusubiria abiria wanaotua uwanjani hapo wakitokea nje ya nchi.
Paparazi wetu alikuwa akimsubiri mgeni wake lakini kama ilivyo kawaida ya wanakikosi cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ alikuwa na zana zake za kazi kama kawaida.
Wakati wageni wakianza kutoka, ghafla zilisikika kelele pembeni mwa sehemu aliyokuwa paparazi wetu, akajiuliza kunani? Akaweka zana zake za kazi sawa kisha akajongea eneo la tukio.
VARANGATI LA NGUVU
Kamera za Risasi Mchanganyiko zilishuhudia wanawake wawili wakikunjana na kupigana makonde huku mmoja akimshutumu mwenzake kumwibia mumewe (haikujulikana kama ni wa ndoa). Alisema: “Wewe mpumbavu mwizi wa waume za watu, nitakukomesha leo. Si umezoea kuiba waume za watu? Sasa utanijua mimi ni nani?”
Mwanamke huyo aliyeonekana kuwa na jazba, alikuwa na watoto wake wawili waliovalia sare za shule ambao walikuwa wakimvuta na kumsihi aachane na ugomvi.
MSHANGAO NI HUU!
Sekeseke wakati likiendelea, yule mwanamke ambaye alikuwa akidai kuibiwa mumewe kwa muda mrefu na mwanamke huyo, watoto wake wawili walikuwa naye sambamba huku wakijaribu kumtuliza ingawa kiumri ni wadogo.
Mwanamke aliyedaiwa kuchukua mume wa mwenzake naye alikuwa na mtoto wake mmoja ambaye alikuwa akimvuta akitaka kumtoa mikononi mwa mwanamke aliyedaiwa kuwa mmiliki rasmi wa tajiri huyo.
Mshangao mkubwa ni kitendo cha watoto hao wote kuwa wamevaa sare za shule, tena zikionekana kuwa za shule moja – maswali yalikuwa mengi kuliko majibu!
“Hawa watoto sijui wamekuja na huyu jamaa? Maana wanaonekana kama wanasoma shule moja na wapo na vifaa vyao vyote vya shule. Hapa hata haileweki jamani,” alisikika dereva teksi mmoja aliyekuwepo eneo la tukio.
MAELEZO MENGINE
Mashuhuda walisema, awali tajiri yule wakati anatoka katika sehemu maalum ya abiria wanaoingia nchini, alikimbiliwa na mwanamke yule anayedaiwa kuwa kimada na kumpokea kisha kumbusu na kumpa pole kwa safari.
“Tatizo lilianzia pale yule mwanamke mwembamba mwenye nguo nyekundu alipoenda kumpokea jamaa. Alimfuata na kumkumbatia kisha akambusu, basi hapo tafrani ikatokea. Yule mke wa jamaa alikwenda haraka na kumvamia kisha kuanza kumpiga,” alisikika mmoja wa mashuhuda hao.
TAJIRI AWAZODOA WALIOMSHANGAA!
Wakati tafrani ile ikiendelea, mwanaume huyo aliwaingilia kati na kuwaamulia, jambo lililozidisha watazamaji wa sinema hiyo ya bure kushangaa.
Katika hali ya kushangaza, tajiri huyo aliwananga watu waliokuwa wakimshangaa akisema: “Sasa kipi cha ajabu? Ni mwanaume gani hapa ambaye hajawahi kufumaniwa? Haya ni mambo ya kawaida, endeleeni na shughuli zenu nitamaliza hii ishu mwenyewe.”
Juhudi za tajiri huyo kuwaachanisha zilizaa matunda, kwani zaidi ya kutumia nguvu, alionesha ‘uanaume’ wake kwa wanawake hao ambao walikubali kuachana na ugomvi huo ingawa kila mmoja alionekana kuwa na hasira na mwenzake.
Baadaye yule mwanamke aliyedaiwa kuwa ndiye mke halali wa tajiri yule, aliondoka naye wakiwa na watoto wao wawili, mwingine akaondoka na mtoto wake.

Endelea Kusoma...